Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
imeipiga faini ya sh. 500,000 (laki tano) mabingwa watetezi klabu ya
Yanga baada ya kitendo cha mashabiki wake kurusha uwanjani chupa
zinazosadikiwa kuwa na mikojo katika mchezo wao dhidi ya watani zao wa
jadi Simba SC.
Kamati hiyo imeikuta klabu ya Yanga na hatia baada ya kupitia ripoti za michezo yote ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Yanga SC inakabiliwa na adhabu hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 42(1) kuhusu udhibiti wa klabu.
Katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara namba 58, mabingwa watetezi
klabu ya Yanga ilishuka dimbani Oktoba 28 kukabiliana na Simba SC
Uwanja wa Uhuru.
Katika mchezo huo wa watani wa jadi uliamuliwa kwa sare ya1-1, wakati
Simba SC ikiwa ya kwanza kujipatia goli kupitia kwa Shiza Ramadhani
Kichuya huku wenyeji Yanga wakisawazisha bao hilo kupitia Obrey Chirwa.