Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza
karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya
Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na
kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.
Moja ya habari iliyoandikwa leo ni hii
kutoka gazeti la Jambo leo yenye kichwa cha habari ‘Sababu za wanandoa
kukimbiana harusini’.
Baada ya kuwepo kwa mfululizo wa wa
matukio ya wapenzi kukimbiana siku ya harusi, gazeti la Jambo leo
limezungumza na mtaalamu wa Saikolojia na uhusiano wa chuo kikuu cha Dar
es salaam, Dk. Chris Mauki amezitaja sababu za watu wengi kukimbiana
siku ya harusi ikiwemo ni pamoja na kutofahamiana vizuri, kuhifadhi vitu mioyoni na wasiwasi juu ya ndoa baina ya wapenzi